Dk Batilda apongeza ubunifu watafiti MUHAS

TANGA: Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Buriani amepongeza na kuonesha kufurahishwa na bunifu zinazotengenezwa na wanafunzi na watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), zinazowasilishwa katika maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Shule ya Sekondari Usagara, Mkoa wa Tanga.

Akiwa katika banda la MUHAS, Mkuu wa Mkoa alitembelea maeneo mbalimbali yanayoonesha bunifu na teknolojia zinazolenga kutatua changamoto katika sekta ya afya na kuboresha huduma kwa jamii.

Alieleza kufurahishwa na namna MUHAS inavyowezesha vijana kutumia elimu na ujuzi walioupata kubuni suluhisho zinazolenga kukidhi mahitaji halisi ya jamii.

Ushiriki wa MUHAS katika maadhimisho hayo unaendelea kutoa fursa kwa wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali kujifunza kuhusu bunifu zinazozalishwa chuoni, pamoja na kupata uelewa kuhusu mchango wa elimu, ujuzi, utafiti na ubunifu katika maendeleo ya taifa.

Kupitia maadhimisho haya, MUHAS inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuibua, kukuza na kuendeleza bunifu zinazolenga kutatua changamoto za jamii, hususan katika sekta ya afya.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button