LICHA ya Tanzania kukabiliwa na uhaba wa watumishi wa Afya katika vituo vya kutoa huduma vya Afya nchini, imeelezwa kwua wafamasia wengi wapo mitaani hawana kazi baada ya kuhitimu mafunzo yao katika vyuo mbalimbali
Rais wa Chama cha Wafamasia nchini(PST), Fadhiki Hezekiah akizungumza leo Septemba 28, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya awali ya siku ya wanafamasia duniani amesema takwimu za shirika la afya Duniani (WHO) limetoa idadi gani ya daktari anafaa kuhudumia wagonjwa wangapi lakini kwa Tanzania bado ni changamoto.
“Madaktari wanatoa huduma kwa wagonjwa wengi kwa siku kutokana na uchache watoa huduma wa afya.”Amesema
|Aidha, ametoa rai kwa serikali kutupia jicho changamoto ya wafamasia kukosa kazi kwa kuwaajiri na kuwapeleka kwenye vituo vya afya wakatoe huduma ili kutatua changamoto hiyo.
Hezekiah, amesema wakati dunia ikiadhimiha siku ya wafamasia bado dunia inashudia ongezeko kubwa la usugu wa Dawa, Ongezeko la matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari, ongezeka la watu kutumia Dawa bila kupima, huku akiwataka watanzania kuacha kutumia dawa bila kufuata ushauri wa Daktari.