IGP apangua makamanda mikoa mitatu

IGP Camillus Wambura

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camilius Wambura, amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi katika mikoa mitatu kwa lengo la kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kwenye mikoa hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa jeshi la polisi, SACP, David Masime leo, Januari 6, 2023 imesema aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP), Fortunata Muslim amehamishwa kwenda kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Aidha IGP Wambura amemteua Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Alex Mukama aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe kuchukua nafasi ya SACP Fortunata Muslim.

Advertisement

Katika marekebisho hayo, IGP amemhamisha Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Shadrack Masija kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.

ACP Shadrack Masija alikuwa Afisa Mnadhimu namba moja Mkoa wa Simiyu.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *