Jaydee amzawadia Diamond kitabu cha maisha yake

DAR ES SALAAM: Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, amemzawadia msanii mwenzake, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, kitabu chake kinachoitwa Diary ya Lady Jaydee.

Lady Jaydee amefanya hivyo baada ya kupata nafasi ya kushiriki chakula cha jioni pamoja na Diamond na watu wengine, huku akieleza kufurahishwa na muda huo wa kushirikiana, kuimba na kufurahia maisha pamoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lady Jaydee alieleza furaha yake kwa kupata nafasi ya kukutana na watu mbalimbali na kushiriki nao wakati mzuri, akiwamo Diamond Platnumz.

Baada ya kukabidhiwa kitabu hicho, Diamond amemshukuru Lady Jaydee na kumpongeza kwa hatua kubwa za mafanikio alizopiga katika safari yake ya muziki.

Diamond pia ameeleza kuwa ana shauku ya kukisoma kitabu hicho, akisema kina umuhimu na maana kubwa katika maisha yake pamoja na safari yake ya muziki.

Kitabu Diary ya Lady Jaydee kinaelezea sehemu mbalimbali za safari ya msanii huyo katika muziki, akiwamo uzoefu, changamoto na hatua alizopitia katika kujenga jina lake katika tasnia ya muziki Tanzania.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button