Rekodi zavunjwa michuano ya Kuogelea

DAR ES SALAAM: REKODI zilizovunjwa na waogeleaji katika Mashindano ya Taifa ya Kuogelea yaliyomalizika jana zimeonesha maendeleo ya mchezo huo nchini, huku vijana wakipewa nafasi ya kujijengea msingi wa kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa.
Akizungumza baada ya mashindano hayo, Katibu wa Mashindano wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Frank Lusawa amesema ushindani mkubwa uliojitokeza na kuvunjwa kwa rekodi ni ishara ya kazi kubwa inayofanywa na waogeleaji, makocha pamoja na wazazi.
“Ushindani ulikuwa mkubwa na tumeona rekodi zikivunjwa. Hii inaonesha kwamba waogeleaji wanaendelea kufanya vizuri na juhudi za makocha pamoja na wazazi wao zinaanza kuonekana,” amesema.
Amesema mashindano hayo pia yamekuwa sehemu muhimu ya kuwahamasisha waogeleaji vijana kuboresha muda wao ili kupata nafasi ya kushiriki mashindano makubwa zaidi na hatimaye kufungua fursa nyingine ikiwamo kupata ufadhili wa masomo.

Lusawa amesema vijana wanapaswa kuunganisha michezo na elimu, kwa kuwa vipaji vya michezo vinaweza kuwa sehemu ya maisha yao ya baadaye, huku elimu ikiwa msingi muhimu wa maendeleo yao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Monti International School, Fatma Fernandes, amesema sekta binafsi ina nafasi kubwa ya kusaidia Serikali na TSA katika kuendeleza mchezo huo, hasa kwa kuongeza miundombinu inayowawezesha waogeleaji kufanya mazoezi na kushindana katika mazingira bora.

Amesema shule hiyo imewekeza katika bwawa la kuogelea lenye urefu wa mita 25 na pia huleta makocha mbalimbali kufanya kazi pamoja na makocha wa Tanzania kwa lengo la kuongeza ujuzi na kuboresha viwango vya ufundishaji wa mchezo huo.
Fernandes amesema uwekezaji huo unaendana na juhudi za kuhakikisha watoto wenye vipaji wanapata mazingira mazuri ya kuendeleza uwezo wao na kufikia viwango vya juu katika michezo.




❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa …………………………………………………………………..………> https://da.gd/girls66