Patel atwaa ubingwa kwa mara ya tatu Afrika

MOROGORO: DEREVA mzoefu Karan Patel na mwongozaji wake Tauseef Khan wameweka rekodi nyingine kwa kuiwakilisha nchi yao kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya tatu wa Afrika Rally Championship katika mashindano ya mbio za magari za Serengeti Rally of Tanzania.
Mahindano ya Serengeti Rally of Tanzania 2026 yamefanyika kwa siku nne hadi 4,2026, kwenye Shamba la Msitu la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS )mkoani Morogoro yakiwa ni sehemu ya kalenda ya African Rally Championship na kushirikisha mataifa ya Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Tanzania.

Patel akitokea kwenye timu ya Asas amesema kufanikiwa kuwa bingwa kwa mara nyingine kumesababishwa na ushindani mkubwa aliopata kutoka kwa Mtanzania Manveer Baldi ambaye wanatokea timu Moja ya Asas.
“Ushindani mkubwa ulionekana katika hatua mbalimbali za mashindano na washiriki wakionesha umahiri, kasi na uzoefu katika kukabiliana na changamoto za njia za rally,” amesema Patel.
Patel amesema ushindani wa mwaka huu ilikuwa mkubwa kutokana na uboreshaji wa miundombinu ya barabara na kwamba matamanio yake ni kushiriki mashindano makubwa zaidi licha ya kukabiliwa na changamoto ya gharama kubwa ya kushiriki mashindano ya kimataifa.

“ Licha ya kufanya vizuri kwenye mashindano haya na kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu fululizo , kitendo hiki kimeniongezea chachu kubwa ya kupiga hatuna zaidi ya kutamani kwenda kushindana mashindano ya Dunia ya Magari” anasema Patel.
Naye mshindi wa pili wa Afrika Rally Championship, Manveer Bardi ambaye pia ni mshindi wa kwanza kwenye National Rally Championship amempongezaPatel kwa ushindi alioupa kwani uzoefu wake wa mashindano hayo ndio ilikuwa kikwazo kwake yeye kuibuka na ubingwa.
“Hii ni mara yangu ya nne kushiriki mashindano najitahidi kufanya vizuri , nimpongeze Patel ni mzoefu sasa huu ni ubingwa wake wa mara tatu, nami sasa ninaniandaa kwa mashindano yatakayofanyika mkoani Arusha, naimani nitafanya viziri,” amesema Bardi.

Katika mashindano hayo ,nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Yasin Nasser kutoka timu ya Ampiano na wengine ni Ahmed Huwel kutoka timu Mkwawa akishika nafasi ya nne, nafasi ya Tano ikanyakuliwa na Oscar Ntambila kutoka Uganda na nafasi ya sita ilitwaliwa na Dk Nsereko Godfrey kutoka Uganda.

Kwa upande wake Dereva Susan Muwonge ambaye alikuwa ni mwanamke pekee na mwongozaji wake Musa Nsubuga kutoka nchini Uganda hakufanikiwa kumaliza mashindano baada ya gari aliyokuwa akiitumia kuharibika.



