Kampeni ya kukuza vipaji yarejea kwa kasi

DAR ES SALAAM: Kampuni ya vinywaji ya Serengeti Breweries kwa kushirikiana na KUNTA Africa imetangaza kurejea kwa kampeni ya Nyota Bigi kwa msimu wa pili, ikiwa na lengo la kuwapa vijana wa Tanzania jukwaa la kuonyesha vipaji vyao, kukuza ubunifu na kujenga fursa kupitia uwezo walionao.
Kampeni hiyo yenye kaulimbiu “Lite Your Imagination” inalenga kuwafikia vijana katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Dodoma, huku shughuli zake zikianza rasmi Dar es Salaam Oktoba 3, 2026, kabla ya kuendelea Mwanza Oktoba 10, Arusha Oktoba 17 na kumalizika Dodoma Oktoba 24.
Akizungumza kuhusu msimu huo, Meneja wa Masoko na Ubunifu wa Serengeti Breweries, Henry Esiaba, amesema Nyota Bigi ni jukwaa linalowawezesha vijana kuonyesha vipaji vyao na kupata fursa zitakazowasaidia katika safari yao ya mafanikio.
Amesema kampeni hiyo inalenga vijana wenye vipaji mbalimbali ikiwemo muziki, uchezaji, uigizaji, uchekeshaji, sanaa na ubunifu mwingine, huku akiwataka kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo kuonyesha uwezo wao.
“Tuna vipaji vingi katika kila kona ya nchi hii, lakini kinachokosekana wakati mwingine ni nafasi ya kuonekana. Nyota Bigi ipo kwa ajili ya kuwapa vijana wa Tanzania jukwaa hilo,” amesema Esiaba.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Bia wa Serengeti Breweries, Rhona Namanya, amesema msimu wa pili wa Nyota Bigi utakuwa mkubwa zaidi kwa kuhusisha shughuli mbalimbali katika miji hiyo, hatua inayolenga kuunganisha vipaji vya vijana na fursa zilizopo katika sekta ya ubunifu.
Amesema hatua hiyo pia inalenga kupanua wigo wa kampeni hiyo kutoka Dar es Salaam pekee na kuwafikia vijana katika maeneo mengine ya Tanzania.
“Mwaka huu tunafurahi kuwahusisha Watanzania kwa msimu wa pili ambao utakwenda katika miji mbalimbali Tanzania, tofauti na mwaka jana ambapo tulifanya shughuli hizi Dar es Salaam pekee,” amesema Namanya.
Aidha, waandaaji wameeleza kuwa usajili wa washiriki utafanyika kupitia msimbo wa QR wa Nyota Bigi pamoja na WhatsApp, ambapo vijana watawasilisha taarifa zao na video fupi zinazoonyesha vipaji walivyonavyo.
Mfumo huo unalenga kurahisisha ushiriki wa vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini na kuwapa nafasi ya kuonekana kupitia jukwaa hilo la ubunifu.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com