Kasulu yaweka mkakati matumizi nishati safi

KIGOMA: Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imetangaza mpango mkakati wa matumizi ya nishati safinya kupikia ili kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Ofisa Maliasili ma Mazingira wa Wilaya Kasulu, Elikana Maige alisema hayo akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Wazo Mwang’onda alipotembelea kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo la wanafunzi la Shule ya Sekondari Makere na mradi wa jiko banifu ambapo alisema kuwa kwa sasa ni aslimi 10 ya wananchi wa wilaya hiyo wanaotumia majiko banifu na sanifu.

Maige alisema kuwa katika mpango wa halmashauri wanatarajia kaya 102,000 katika halmashauri ya wilaya Kasulu mkoani Kigoma kutumia nishati safi ya kupikia kufiki mwaka 2030.

Kutokana na hilo alisema kuwa halmashauri inatekeleza mipango mbalimbali ya uhifadhi mazingira ikiwemo kupanua hifadhi za misitu za vijiji, kugawa majiko banifu 3570 kwa kaya masikini kwa vijiji 14, kugawa mitungi ya gesi ya ruzuku 1624, kutoa elimu ya utengenezaji wa majiko banifu na mkaa mbadala.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa, Wazo Mwang’onda alisem kuwa matumizi ya nishati safi ni ndoto ya Rais Samia kuona wananchi wote wa Tanzania wanatumia nishati safi kuepukana na uharibifu wa mazingira.

Mwang’onda alisema uharibifu wa mazingira una athari katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutokana na kuvurugika kwa mifumo ya hali ya hewa na kusababisha athari za mabadilko ya tabia nchi hivyo kuwepo kwa ukame, mafuriko na vimbunga na kwamba ni wajibu wa kila Mtanzania kutumia nishati safi ya kupikia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button