Katekista kortini akidaiwa kunajisi mtoto

JESHI la Polisi mkoani Geita, limemfikisha mahakamani kiongozi wa dini (Katekista), Athanas Rugambwa (62), mkazi wa kijiji cha Mganza wilayani Chato mkoani hapa, akidaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka nane.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Henry Mwaibambe amesema kiongozi huyo wa dini anatuhumiwa kutenda kosa hilo Agosti 4, 2022, kwa mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu.
“Tulimfikisha jana (Septemba 14) kwenye mahakama ya Wilaya ya Chato,” amesema.



