Kocha Singida akubali Yanga inatisha
KOCHA wa Singida Big Stars Hans Van Pluijim, amesema hana cha kuwalaumu wachezaji wake kwa kupoteza mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam kwa kutandikwa bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Liti mkoani Singida.
Kocha Hans amesema Yanga wana ubora mkubwa kwa sasa na ndio maana wapo kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo ubora wao ndio ulioamua mchezo wa leo licha ya kwamba wachezaji wake walipambana dakika zote 90.
Kocha huyo Mholanzi anasema licha ya kuikamata Yanga kwa zaidi ya dakika 80 za mchezo huo, lakini uwezo binafsi wa nyota Fiston Mayele ulitofautisha mchezo huo.