Mambo yamenoga tamasha la Nyangumi

MTWARA: Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya, amewataka wananchi mkoani Mtwara kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika Tamasha la Nyangumi Festivali 2026 msimu wa nne.

Tamasha hilo lililokutanisha wananchi, wadau na sekta mbalimbali ikiwemo za umma na binafsi limezinduliwa rasmi leo Septemba 3 mwaka huu na kuhitimishwa Septemba 5, mwaka huu.

Tamasha hilo hufanyika kila mwaka kutokana na uwepo wa kivutio cha nyangumi wanaofika katika maeneo ya bahari ya Mtwara katika ghuba ya Mnazi Bay iliyopo kijiji cha Msimbati Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Akizungumza katika uzinduzi huo mkuu huyo wa wilaya amesema nyangumi hao hufika kwenye maeneo hayo kwa ajili ya shughuli zao za kawaida ikiwemo kuzaliana hatua ambayo ni fursa kwa wananchi na wageni kutoka maeneo mbalimbali kuja kujifunza na kutambua umuhimu wa uhifadhi wa bahari na rasilimali zake.

“Siku hii ni adhimu na muhimu sana kwetu wanamtwara na ni jambo kubwa ambalo lipo katika mkoa wetu na si tu mkoa wetu tunajivunia sana jambo hili kuwepo katika wilaya yetu ya mtwara”amesema Mwaipaya

Nae Mhifadhi Mfawidhi wa Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma Dk. Redfred Ngowo amesema lengo kubwa la tamasha hilo ikiwemo kukuza utalii wao katika ukanda huo wa kusini.

Baadhi ya wadau mkoani humo akiwemo Meneja wa Shirika lisilo la kiserikali la TRADE AID mkoani humo Emmanuel Mwambe ameuomba uongozi mkoani humo kuwe na kamati ya udumu itayosimamia matamasha hayo ili wasiwe wanajirudia kila mwaka kuanza maandalizi tena.

Hata hivyo Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Dk. Emmanuel Sweke amesema moja ya majukumu yao ni kuhakikisha wanahifadhi rasilimali za bahari na kuwezesha kuzalisha zaidi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button