Mauzo ya mazao yaongezeka asilimia 43.6

KIASI cha mazao yaliyouzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kimeongezeka kwa asilimia 43.6 katika mwaka wa fedha 2025/26.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Julai 31, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Asangye Bangu, amesema ongezeko hilo ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi kwa mwaka wa fedha 2025/26, huku akieleza mwelekeo wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2026/27. SOMA: TADB yaendelea diplomasia ya uchumi kupitia kilimo
Amebainisha kuwa jumla ya kilo bilioni 1.122 za mazao ziliuzwa kupitia mfumo huo ikilinganishwa na kilo milioni 781.6 zilizouzwa mwaka uliopita. Amesema ongezeko hilo linaonyesha kuendelea kuongezeka kwa uaminifu wa wakulima na wadau wa kilimo kutumia mfumo rasmi wa biashara ya mazao. Ameeleza kuwa WRRB itaendelea kupanua matumizi ya mfumo huo ili kuwafikia wakulima wengi zaidi na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko mbalimbali.




I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. https://www.work27.info