Mvua yaharibu miche ya kahawa Mbozi

MVUA iliyoambatana na upepo mkali pamoja na mawe imeharibu zaidi ya miche 100,000 ya zao la kahawa pamoja na mazao mengine katika vitongoji vinne katika kijiji Cha Ndolezi kata ya Mlangali wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Mwenyekiti wa kijiji cha Ndolezi, Ezekia  Tim amesema mvua hiyo iliyonyesha Februari 15, 2025 majira ya saa nane mchana imeharibu pia mazao ya parachichi ,mahindi , alizeti, karanga na mbogamboga .

“Zao la kahawa pekee ni zaidi ya miche laki moja imeharibiwa vibaya kwa kupukutisha punje na majani kuharibika vibaya, tunaiomba serikali , bodi ya kahawa, wadau wa kahawa na watalaam kuja kutembelea ili waone namna ya kutusaidia  hali ni mbaya kwa wananchi wangu,”amesema.

Advertisement

Amevitaja vitongoji vilivyopata madhara zaidi katika kijiji hicho kuwa ni Ndolezi A, Ipota, Ndolezi B na Sazule, … vijiji jirani vilivyopata madhara ni Mlangali , Masoko na Nambala kwa kiasi kidogo.

Ofisa kilimo kata ya Mlangali, Regina Kololo amesema kutokana na madhara hayo ya mvua katika kata hiyo watayazungukia maeneo yote yaliyoathiriwa kwa ajili ya kufanya tathmini, ambapo baada ya tathmini watakutana na wananchi kwa ajili ya ushauri zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *