Polisi yachunguza sanduku lililozua taharuki stendi ya daladala

DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa tukio la kuonekana kwa sanduku la mbao lililotelekezwa kituo cha daladala ziendazo Tegeta, eneo la Mwenge wilayani Kinondoni, ambalo lilizua taharuki miongoni mwa wananchi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, tukio hilo limetokea leo Agosti 6, 2026 majira ya saa 3 asubuhi.
Amesema sanduku hilo lilikuwa limetengenezwa kwa mbao, mlango wake ukiwa umefungwa kwa kufuli na kuzungushiwa kipande cha kitambaa kwa mtindo wa jumlisha, huku likiwa limetelekezwa na mtu au watu wasiojulikana.
“Hali hiyo ilisababisha taharuki na hisia mbalimbali kwa wananchi waliovutika katika eneo hilo,” alisema SACP Muliro.
Aliongeza kuwa baada ya kupokea taarifa, timu ya wachunguzi kutoka Jeshi la Polisi ilifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa awali kabla ya kulifungua sanduku hilo.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, ndani ya sanduku hilo kulikutwa kipande cha mbao kilichochongwa kwa mfano wa mguu wa kiti au kitanda cha mbao cha mtindo wa kizamani.
Kamanda Muliro alisema tukio hilo linaweza kuhusishwa na imani za kishirikina au kuwa na nia ya kuzua taharuki miongoni mwa jamii, huku uchunguzi zaidi ukiendelea kubaini waliohusika na sababu za kulitelekeza sanduku hilo eneo hilo.




Heya! I’m at work surfing around your blog from my new iphone 3gs!
Just wanted to say I love reading through your blog and
look forward to all your posts! Keep up the great work!
I do not know if it’s just me or if everyone else encountering issues with your website.
It appears as if some of the written text on your content are running off the screen. Can somebody else please comment and
let me know if this is happening to them as well?
This might be a problem with my web browser because I’ve had this happen previously.
Thank you
I have read so many articles regarding the blogger lovers
except this piece of writing is truly a nice paragraph, keep it up.
Post writing is also a excitement, if you know after that you can write or else it is difficult to write.
Hello everyone, it’s my first pay a visit at this web site,
and paragraph is in fact fruitful in favor of me, keep up posting such content.
Hello there! This blog post could not be written much better!
Going through this post reminds me of my previous roommate!
He always kept talking about this. I’ll forward this information to him.
Pretty sure he’s going to have a good read. Thanks
for sharing!