RC ataka droni itumike katika zao la pamba

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha amesema njia ya utumiaji ‘drone’ ( ndege nyuki) kwa unyunyuziaji wa dawa kwenye zao la pamba inaonekana kuleta unafuu kwa wakulima.

Macha amesema hayo alipowatembelea wakulima wa zao la pamba wilayani Kishapu mkoani Shinyanga huku akieleza mashamba yanayoanzia ekari kumi nakuendelea wapewe kipaumbele katika utumiaji wa drone kwenye unyunyuziaji dawa.

Macha amesema kitaalamu drone ikisetiwa vizuri inauwezo wa kunyunyuzia ekari moja kwa dakika sita hivyo jitihada zinatakiwa kufanyika kwa kila mkulima kunyunyuziwa dawa shamba lake na kuu wadudu wanao nyemelea.

Advertisement

‘Serikali imeweka kipaumbele katika kilimo na maafisa ugani wamewekwa kuanzia ngazi ya vijiji na wamepewa vitendea kazi hizi zote ni jitihada za Rais Samia Suluhu katika mikakati ya kuwakomboa wakulima kuinuka kiuchumi”amesema Macha.

Msimamizi wa zao la pamba kutoka Bodi ya Pamba wilayani Kishapu Thadeo Mihayo amesema kwa mkoa wa Shinyanga zipo drone saba lakini mipango iliyopo kupata zingine ili kufikia drone 14.

Mihayo amesema watatekeleza suala la kipaumbele kwa wakulima wenye ekari nyingi ambapo wanatakiwa kuandaa maji kwaajili ya kuchanganyia dawa ila vifaa vingine na dawa ni juu ya bodi ambayo inasimamia.

Mkulima kutoka kijiji cha Kinampanda kata ya Mwamalasa Ngusa Mayunga amesema amelima ekari kumi amesimamiwa na wataalamu wa kilimo nakufuata kanuni bora ya ulimaji wa zao hilo kwanza kutochanganya mazao mengine.

Mayunga amesema kipindi hiki nichakunyunyuzia dawa amekuwa akitumia pampu kwa kuibeba mgongoni wakati mwingine anachoka nakutumia muda wa siku mbili au tatu kukamilisha shamba lote.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *