Serikali kuweka mazingira wezeshi elimu

MTWARA: SERIKALI imesema itahakikisha inaendelea kuweka mazingira wezeshi
kwa wananchi ili wayafikie maendeleo ikiwemo suala zima la elimu.

Akizungumza mkoani Mtwara katika Halmashauri ya Mji Newala, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga,  amesema kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa hao ili waweze wayafikia maendeleo na kuwapatia elimu bora.

Hayo yamejiri wakati waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi katika halmashauri hiyo kwa lengo la kukagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya mcholi 1 iliyopo kwenye halmashauri hiyo iliyogharimu zaidi ya Sh milioni 560.

Hata hivyo waziri huyo wa viwanda na biashara amepata fursa ya kuzungumza na wananchi wa halmashauri hiyo kupitia mkutano wa hadhara uliyofanyika kwenye shule hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Newala Rajabu Kundya ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujenga miundombinu ya madarasa pamoja shule mpya kwenye kwenye halmashauri hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Abilahi Mniha ameelezea namna ambavyo serikali inatekeleza kwa vitendo ahadi zake kwa wananchi.

“Rais amejibu hitaji la wananchi kupitia ujenzi wa shule hii hakika yeye ni kiongozi mtendaji anayependa matokeo ya hatua za maendeleo kwa wananchi”amesema Mniha

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button