Tanzania yafuzu hatua ya pili Kriketi

TANZANIA imefuzu hatua ya pili michuano ya Afrika ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kuitandika Ghana kwa mikimbio 88 kwa wiketi tatu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Leo.

Awali, Ghana iliongoza kwa mikimbio 84 kwa wiketi tisa lakini Tanzania ikaipiku kwa ubora.

Ushindi huo ni wa tatu mfululizo, baada ya kufanya vizuri katika michezo mingine dhidi ya Lesotho, Malawi na Mali na kufikisha jumla ya pointi nane kwenye uongozi wa kundi A.

Katika kundi hilo, timu nyingine inayopewa uwezekano wa kuungana na Tanzania ni Malawi iliyokuwa na pointi sita anayetarajia kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya Cameroon. Pia, Mali itacheza dhidi ya Lesotho.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo Atif Salim, timu mbili kwenye kundi hilo, zitakutana na timu nyingine nne kutoka kundi B na C ambapo zitacheza kutafuta nafasi mbili za kuwakilisha Kombe la Dunia.

“Kwenye makundi matatu, kuna timu sita zitaungana na timu mbili ambazo tayari zilishafuzu yaani Uganda na Namibia zitakuwa nane zitacheza hatua ya mwisho na mbili zitakazofanya vizuri zitawakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia,”amesema.

Katika mchezo huo wa Tanzania na Ghana, mchezaji aliyefanya vizuri ni Akhil Anil aliyehusika kwa kiasi kikubwa kwenye ushindi wa timu.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button