Tanzania yavuna mikataba mitatu Africa50

TANZANIA  imehitimisha kwa mafanikio Jukwaa la Miundombinu Afrika na Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Africa50, huku mikataba na makubaliano matatu muhimu katika sekta za umeme, gesi na afya yakisainiwa ili kuimarisha uwekezaji na maendeleo ya miundombinu nchini.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Africa50 uliofanyika katika  jijini Dar es Salaam,Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar amesema  jukwaa la siku mbili lililoanza Agosti 5, 2026 na kufunguliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan limekamilika kwa mafanikio, likifuatiwa na Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Africa50 aliouongoza kwa pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Sidi Ould Tah

Amesema katika jukwaa hilo wamekubaliana makampuni mawili kushirikiana ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Africa50 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya usafirishaji wa umeme.SOMA: ETDCO yakamilisha mradi wa umeme kabla ya muda

Makubaliano ya pili ambayo ymepepitishwa  kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Taqa Arabia kwa ajili ya kuendeleza mradi wa mini LNG utakaosaidia upatikanaji wa gesi kwa matumizi ya viwanda.“Huu si ule mradi mkubwa wa LNG wa Lindi, bali ni mradi mdogo wa kuchakata na kutumia gesi kwa mahitaji ya viwanda,” alisema.

Balozi Omar  amesema makubaliano ya tatu yanahusu ujenzi wa kituo kipya cha usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo (dialysis) ili kuboresha huduma za matibabu nchini. SOMA: Wananchi wanufaika uchunguzi wa afya bure, dawa asili MUHAS

Amesema ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza hususan yanayohusiana na figo na mfumo wa mkojo, limeifanya Serikali kuona umuhimu wa kuongeza vituo vya dialysis.”Tumebaini kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanaongezeka, hivyo ujenzi wa vituo vya ziada vya usafishaji damu ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi,” alisema.

Balozi Omar amesema hatua zilizofikiwa kupitia jukwaa hilo zinaonyesha kuongezeka kwa imani ya taasisi za fedha za maendeleo na sekta binafsi katika kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati nchini na barani Afrika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button