TBS yateketeza tani 39 bidhaa zisizokidhi viwango

DAR ES SALAAM; Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeteketeza tani 39 za bidhaa za chakula zisizokidhi matakwa ya viwango, zenye thamani ya takribani Sh milioni 149.

Tukio hilo limefanyika leo, Agosti 17, 2026, Mbezi Gongoni, Wilaya ya Mkuranga, Pwani, baada ya bidhaa hizo kubainika kupitia ukaguzi uliofanyika katika kipindi cha Julai hadi Agosti.

Kwa mujibu wa taarifa ya TBS, baadhi ya bidhaa hizo, hazikuwa na alama ya ubora, zilikosa maelezo sahihi kwenye vifungashio, zilikuwa hazina taarifa kwa Kiswahili au Kiingereza kama inavyotakiwa na baadhi zilikuwa zimekwisha muda wa matumizi.

Taarifa ya TBS imewasisitiza wafanyabiashara kuhakikisha bidhaa wanazoingiza au kuuza zinakidhi viwango vilivyowekwa, huku wananchi wakihimizwa kusoma maelezo ya bidhaa na kuangalia alama ya ubora kabla ya kununua au kutumia.

“Hatua hii ni sehemu ya juhudi za TBS kulinda afya za wananchi na kuhakikisha bidhaa salama na zenye ubora zinafika kwa watumiaj,” imesema taarifa hiyo..

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button