TLS wakata kauli ya serikali kukamatwa vyombo vya dola

LINDI: CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Ipilinga Panya amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa kauli ya katazo kwa vyombo mbalimbali vya dola ambavyo vimekuwa vikiwakamata Mawakili na kuwasweka rumande bila kuwa na hatia kwa madai ya kuingilia shughuli zao.

Pia amesihi kuagizwa uwajibishwaji kwa maofisa hao wa vyombo vya dola kwani wanafifisha jitihada na kampeni za Rais Samia Suluhu Hassan za kutaka wananchi kufikiwa na misaada mbalimbali ya kisheria na utetezi pale wanapokuwa na masuala yanayohusu mahakama na sheria.

Ipilingi ameeleza hayo leo Februari 19,2025 akimuwakilisha Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika uzinduzi ya kampeni hiyo Mkoani Lindi, kampeni inayozinduliwa wilayani Ruangwa,

Wakili Ipilinga amezitaja baadhi ya Taasisi hizo ambazo zimekuwa zikiwakamata Mawakili wawapo kwenye shughuli zao kuwa ni pamoja na Polisi, Jeshi la uhamiaji, Mamlaka ya udhibiti wa dawa za kulevya, Taasisi kudhibiti na kuzuia rushwa Tanzania (TAKUKURU) pamoja na nyinginezo ambazo zimekuwa zikiwakamata kwa madai kuwa Mawakili wanaingilia shughuli zao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button