DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu), Williamu Lukuvi amesema ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya Maji Kata ya Mbezi ni kielelezo tosha kinachoonesha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo.
Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea Miradi ya Maendeleo ambapo ametembelea na kujionea Mradi wa Maji Mshikamano ulipo Kata ya Mbezi Katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar e salaam na baadae kufanya Mkutano wa hadhara Mburahati, leo tarehe 18/09/2023.
Shida ya maji Kata ya Mbezi ilikuwa tatizo kubwa hivyo kukamilika kwa Mradi wa Maji niliotembelea kwa 100% utahudumia watu zaidi ya laki mbili.
“Rais Dk, Samia Suluhu Hassan ametegua kitendawili hicho kwa Wananchi wa Ubungo kupata Maji safi na salama ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake hivyo niwape shime Wananchi muendelee kutangaza kazi njema zinazofanywa na Serikali,” amesema Waziri Lukuvi.
Kazi hizi zinazofanywa na Serikali zinapaswa kuonekana na kutangazwa ili Watanzania wengine waone kazi mbalimbali kwa mifano na Falsafa ya Mhe. Rais ya Kazi iendelee inaendelea kutekelezwa kwenye miradi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo Ubungo amesema kupitia mradi wa Metroplitan Development Project (DMDP) Awamu ya Pili utajenga kingo za Mto Gide na Mto China huko Makurumula.
Aidha kwa kupitia Mradi wa (DMDP) kwa upande wa Ubungo kuna barabara 21 zitakazojengwa ikiwemo barabara nne kubwa katika Kata ya Kimara ambazo ni barabara ya lami Suka, Barabara ya Mlingo, barabara ya Milenia ya tatu, amesema Waziri Kitila.
SOMA : Aweso aonya mfumo wa GePG huduma za maji
Naye Issa Mtemvu Kibamba amesema Wilaya ya Ubungo ilikuwa na wastani mdogo wa upatikanaji wa maji, lakini Rais amechukua kilio cha wakazi wa Ubungo na leo miradi imekamilika.
“Serikali haikuwaacha Wananchi wa Goba na viunga vya Salasala katika ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye ujazo wa lita zaidi ya milllioni sita eneo Tegeta A hivyo tunamshukuru sana Rais, Dk. Samia,” amesema Mtemvu.