Wachezaji Simba wawaangukia mashabiki
NAHODHA wa Simba, John Bocco amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa kushindwa kupata ushindi kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na HabariLEO, nahodha huyo ameeleza kuwa uchovu na kukosa muda wa kutosha wa mapumziko ni moja ya sababu iliyofanya wasing’are, lakini bado hawajakata tama.
“Ni matokeo mabaya ambayo yanawaumiza mashabiki wetu, lakini hata sisi wachezaji hatuyafurahii, tunaomba watuvumilie na kutuunga mkono sababu ni jambo la mpito,” amesema Bocco.
Sare ya bao 1-1 jana dhidi ya Azam FC, imeifanya timu hiyo kupitwa kwa pointi tano dhidi ya vinara wa ligi hiyo Yanga, ambao jioni ya leo watashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na KMC. Simba ipo mbele mchezo mmoja.