Wachochezi migogoro ya wananchi kukiona

TIMU ya watoa huduma wa msaada wa Kisheria kupitia kampeni ya “Samia Legal Aid Campaign ” imeagizwa kuorodhesha majina ya watumishi wa serikali katika sekta mbalimbali watakaobainika kutajwa na wananchi kuwa wanachochea migogoro inayopelekea wananchi kuichuki serikali.

Aidha timu hiyo iliyosheheni wataalam wa sheria, maofisa maendeleo ya jamii wameagizwa kusikiliza kwa makini wananchi watakaojitokeza kwenye halmashauri saba watakaojitokeza katika kila kata 10 na vijiji vitatu ambavyo timu hiyo itakawanywa kwaaajili ya utatuzi wa changamoto mbalimbali za msaada huo wa kisheria.

Maagizo hayo yametolewa leo jijini Arusha na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda wakati akiongea na wataalam wa sheria wakiwemo mawakili, maofisa maendeleo ya jamii pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali waliokutana kwaaajili ya kupanga mikakati ya utatuzi wa changamoto za wananchi katika halmashauri saba za Mkoa wa Arusha pamoja na kuanisha changamoto zinazopaswa kufanyiwa kazi katika kila idara husika.

Amesema kunabaadhi ya maofisa maendeleo ya jamii wanalalamikiwa kwa kupindisha sheria ikiwemo watumishi wengine hivyo katika kampeni hiyo endapo kunawatumshi wanalalamikiwa kukwamisha utatuzi wa migogoro kwa wananchi  wakuu wa timu husika kutoka Wizara ya Katiba na Sheria waandike majina yao kisha mwisho wa kampeni hiyo watoe taarifa kwake ili hatua stahiki zichukuliwe.

Naye Ester Msambazi ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria,alisema kampeni hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2023 huku mkoa wa Arusha ukiwa ni wa 23 tangu kampeni hiyo ilianza na wamejipanga vema kuanza kutoa msaada huo kuanzia

Ameseema wananchi wanahitaji kusikilizwa kwa kina ikiwemo  kupata haki zao  na Machi 29, mwaka huu timu hiyo itasambaa kwenda uwandani  ambapo watasambaa kwa kila halmashauri huku kata kumi zitafikiwa,  vijiji vitatu vilivyopo kwenye kata hizo zitafikiwa pia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button