Waganga walivyojisajili Baraza Tiba Asili na Tiba Mbadala

MBEYA; Picha za matukio mbalimbali ya waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wakisajiliwa katika Banda la Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, kwenye maandimisho ya Wiki ya Tiba ya Asili ya mwafrika yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya
Usajili wa watoa huduma hao umeelezwa kuwa miongoni mwa hatua zinazoongeza uaminifu wa Jamii na kuimarisha utoaji wa huduma za tiba asili huku tafiti za kisayansi zinazofanywa kuhusu tiba hiyo zikielezwa kuongeza matumizi ya dawa za asili nchini.

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limetoa wito kwa watoa huduma hizo kuhakikisha wanasajiliwa kwa mujibu wa sheria,hatua inayosaidia kuongeza uwazi, uaminifu na usalama wa huduma wanazotoa kwa wananchi.



