Wakulima 2000 kunufaika Skimu ya Umwagiliaji Mto wa Mbu

RUSHA; Zaidi ya wakulima 2,000 Wilaya ya Monduli mkoani Arusha wanatarajiwa kunufaika na ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Bonde la Mto wa Mbu, mradi unaolenga kuimarisha kilimo endelevu cha mazao ya chakula.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, wakati akisoma taarifa ya mradi huo kwa Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, alipotembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi.

Amesema skimu hiyo itahudumia zaidi ya ekari 10,000 na kuwahudumia zaidi ya wakulima 2000 na itajumuisha ujenzi wa barabara za ndani ya mashamba ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na pembejeo za kilimo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Chongolo licha ya kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, ameielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha inalinda miundombinu yote ya umwagiliaji kwa kujenga uzio katika maeneo muhimu na kuelekeza njia za maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo.

Aamewataka wananchi kutunza miundombinu, vyanzo vya maji na mazingira ili kuhakikisha mradi huo unakuwa na manufaa ya kudumu kwa wakulima na wakazi wa maeneo hayo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button