Wakulima wawezeshwa kufikia masoko

SHIRIKA lisilo la kiserikali la INADES-Formation Tanzania limesema linaendelea kutekeleza kaulimbiu ya Maonesho ya Kilimo Nanenane Kitaifa 2026 ya “Tambua Soko, Ongeza Tija, Tekeleza Dira ya Taifa 2050” kwa kuwawezesha wakulima na wafugaji kupata elimu ya kifedha, kuongeza uzalishaji na kuwaunganisha na masoko ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kilimo Nanenane Kitaifa yanayoendelea jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa INADES-Formation Tanzania, Jacqueline Nicodemus, amesema shirika hilo limejikita katika kuhamasisha matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira katika sekta za kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kuboresha maisha ya wananchi.
Amesema INADES inalenga kuwawezesha wakulima na wafugaji kuzalisha kwa ufanisi, kuongeza thamani ya mazao na mifugo yao, pamoja na kuwafungulia fursa mbalimbali za masoko ili kuboresha kipato na maendeleo ya kiuchumi ya jamii.SOMA: Wakulima 2000 kunufaika Skimu ya Umwagiliaji Mto wa Mbu
Nicodemus amesema shirika hilo limepanua wigo wa shughuli zake kwa kuhamasisha wakulima kujihusisha pia na ufugaji, badala ya kutegemea uzalishaji wa mazao pekee, hatua inayolenga kuongeza vyanzo vya mapato kwa kaya. Aidha, amesema INADES hutoa mafunzo kupitia mifumo ya masafa, vitabu na machapisho mbalimbali yanayowasaidia wakulima na wafugaji kujifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji wenye tija.
Kwa upande wa utekelezaji wa miradi, amesema shirika hilo linaendelea kuwekeza katika kilimo, ufugaji, uhifadhi wa mazingira na uendelezaji wa fursa za kiuchumi kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali katika wilaya, mikoa na vijiji nchini.
.Ameeleza kuwa kwa sasa INADES-Formation Tanzania inatekeleza shughuli zake katika mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa, ikihudumia vijiji 26 na kuwafikia zaidi ya wananchi 150,000 kupitia vikundi vya wakulima, taasisi mbalimbali na wakulima mmoja mmoja.

Amesema ushiriki wa shirika hilo katika Maonesho ya Kilimo Nanenane unalenga kuendelea kutoa elimu kuhusu kilimo endelevu, ufugaji wenye tija, uhifadhi wa mazingira na matumizi ya teknolojia zinazoongeza uzalishaji, sambamba na kuimarisha fursa za kiuchumi kwa wananchi.
Nicodemus amesema shirika hilo limepanua wigo wa shughuli zake kwa kuhamasisha wakulima kujihusisha pia na ufugaji, badala ya kutegemea uzalishaji wa mazao pekee, hatua inayolenga kuongeza vyanzo vya mapato kwa kaya. Aidha, amesema INADES hutoa mafunzo kupitia mifumo ya masafa, vitabu na machapisho mbalimbali yanayowasaidia wakulima na wafugaji kujifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji wenye tija.
Kwa upande wa utekelezaji wa miradi, amesema shirika hilo linaendelea kuwekeza katika kilimo, ufugaji, uhifadhi wa mazingira na uendelezaji wa fursa za kiuchumi kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali katika wilaya, mikoa na vijiji nchini. Ameeleza kuwa kwa sasa INADES-Formation Tanzania inatekeleza shughuli zake katika mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa, ikihudumia vijiji 26 na kuwafikia zaidi ya wananchi 150,000 kupitia vikundi vya wakulima, taasisi mbalimbali na wakulima mmoja mmoja.



