Wananchi watakiwa kujitokeza msaada wa kisheria Arusha

MWANANCHI wametakiwa kujitokeza ndani ya kata 10 za jiji la Arusha kueleza changamoto zao zinazohitaji msaada wa kisheria.
Akizungumza leo katika mtaa wa Kalimaji kata ya Moshono jijini Arusha Wakili Moses Matiko amesema endapo wananchi wakitoa changamoto zao kupitia kampeni hiyo watatatuliwa changamoto zao.

Wakali huyo ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Kampasi ya Mwanza na mratibu wa zoezi hilo amesema endapo kutakuwa na changamoto za haki za binadamu mhusika atapelekwa kitengo husika na si lazima kufika mahakamani.
“Changamoto zinazoibuliwa na wananchi tunazichukua na kuzirikodi ikiwemo ukatili wa kijinsia ambao umeibuka kuwa mwingi haswa kwa wanaume ambao hatuongei bali tunakufa kimya kimya hivyo msione aibu wanaume kutoa taarifa ili msikose amani mkakimbia nyumba zenu haswa ukatili huu wa kisailolojia unaoathiri afya zetu wanaume, njooni tuwasikilize ili tuishi katika jamii inayostarabika,”

Kampeni hiyo kwa jiji la Arusha inafanyika kata 10 ambazo ni Moshono, Orolien, Lemara ,Terrat, Murriet, Sokoni one, Olasiti, Sombatini, Kimandolu na Levolosi ambapo kila kata inatoa msaada huo kwa siku moja.



