‘Wapeni elimu ya pensheni kabla hawajastaafu’

‘Wapeni elimu ya pensheni kabla hawajastaafu’

MIFUKO ya hifadhi ya jamii nchini, imetakiwa kutoa elimu ya pensheni kwa watumishi kabla hawajastafu.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi wa semina ya waajiri na viongozi wa matawi ya TUGHE mahali pa kazi.

Katambi amesema mafunzo bora ya utumiaji wa pensheni, yataleta manufaa sana kwa wafanyakazi wanaostafu na kueleza kuwa wafanyakazi au watumishi wanatakiwa kuacha kutegemea tu mishahara, pia wanatakiwa kufanya biashara.

Advertisement

Amesema kumekuwa na taasisi au mashirika yanalipa vizuri sana wafanyakazi wao, lakini wafanyakazi wamekuwa hawafanyi kazi kwa ufasaha na ufanisi kama inavyotakiwa.

Mkutano huu umekutanisha watumishi mbalimbali zaidi ya 800, kutoka serikalini na sekta binafsi.