Watanzania wahamasishwa kutumia vyakula vya asili

LINDI; NAIBU Waziri wa Kilimo David Silinde amewaasa Watanzania kutumia vyakula vya asili ili kuhamasisha matumzi endelevu ya mbegu za asili kwenye kilimo nchini.

Silinde ametoa rai hiyo katika maadhimisho ya siku ya mbegu na chakula asili yaliyofanyika katika viwanda wa Gongo Nanenane Mkoani Lindi.

“Wizara ya kilimo inatoa rai kwa Watanzania sio tu hapa Kusini, kuwa na mazoea ya kutumia vyakula vya asili ili kuhamasisha matumizi endelevu ya mbegu za asili na kuwa na kilimo endelevu,”amesema.

Silinde amesema utumiaji wa vyakula vya asili utasaidia pia kuboresha mifumo ya chakula na kuimarisha maisha ya wakulima nchini Tanzania.

Maadhimisho ya Siku ya Mbegu na Chakula cha Asili yameandaliwa na SWISSAID Tanzania kwa kushirikiana na washirika wake kupitia mradi wa kilimo Ikolojia unaoitwa CROPS4HD.

Mradi huo unatekelezwa na SWISSAID kwa kushirikiana na Alliance for Food Sovereignty in Africa.

Mkurungenzi wa SWISSAID Tanzania, Betty Malaki amesema maadhimisho ya siku ya mbegu na chakula cha asili yanafanyika kwa mara ya tano mkoani Lindi.

Akizungumzia Mradi wa kuendeleza matumizi ya mbegu za asili, Malak amesema umewahusisha wakulima zaidi ya 8000.

Amesema kupitia mradi huo SWISSAID Tanzania na washarika wake wameanzisha benki 15 za mbegu za asili katika Mkoa wa Mtwara na Lindi.

“Tafiti zilizofanywa na SWISSAID zimeonesha kuwa mradi ulichangia kupunguza kwa uhaba wa chakula katika mikoa ya Lindi na Mtwara,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button