Watatu wahukumiwa kunyongwa Musoma

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Musoma mkoani Mara, imewahukumu washtakiwa watatu adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji.

Washtakiwa hao ni Zacharia Werema Matoso ,51,, Daniel Bhoke Ngoko ,46, na Emmanuel Mniko Mwita ,44,, ambao ni wakazi wa Kijiji cha Nkongore, wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.

Katika taarifa iliyotelewa na Jeshi la Polisi imesema kuwa mwendesha mashtaka wa serikali, Lusako Mwaisaka, alieleza mahakama kuwa washitakiwa walitenda kosa la mauaji mnamo Juni 13, 2021. Inadaiwa kuwa walimshambulia Marigore Marwa ,25, mkazi wa kijiji cha Nkongore na kumsababishia kifo, wakimtuhumu kuwa ni mwizi wa mifugo.

Hukumu hiyo ilitolewa Februari 24, 2025, na Jaji M. L. Komba, ambaye alithibitisha kuwa upande wa mashtaka umeweza kuonesha wazi hatia ya washtakiwa wote watatu.

Jaji Komba alieleza kuwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa imetolewa kama fundisho kwa jamii na kwa wote wanaojichukulia sheria mkononi, kwani matendo kama hayo ni hatari kwa ustawi wa jamii.

Hukumu hii inatoa ujumbe mkali kwa jamii kuwa vitendo vya ukatili, hasa kwa kuhusisha mauaji, vitachukuliwa kwa uzito na kutoa adhabu kali kwa wahusika, ili kuzuia matukio kama haya kujirudia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button