Fasili ya bangi yapendekezwa kujumuisha majani, mbegu

DODOMA; Serikali imewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026) ambapo sheria 21 zinapendekezwa kufanyiwa marekebisho.

Akiwasilisha muswada huo leo Septemba Mosi, 2026, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari ametaja miongoni mwa sheria zinazopendekezwa kurekebishwa ni Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95.

“Kifungu cha 2 kinapendekezwa kurekebishwa kwa kuongeza wigo wa fasili ya bangi ili kujumuisha majani na mbegu.

“Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kutambua majani na mbegu kuwa bangi ili kuwezesha utekelezaji wa sheria hususani wakati wa ukamataji, upimaji na uchunguzi wa sampuli au vidhibiti.

“Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 11 kinapendekezwa kurekebishwa kwa kubainisha kosa la kukutwa na mbegu za mmea wowote uliokatazwa pasipo kujali dhumuni la matumizi ya mbegu husika ikijumuisha uzalishaji wa dawa za kulevya.

“Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kupanua wigo wa kosa la kumiliki na kusambaza mbegu za mimea iliyokatazwa na sheria,” amesema Johari.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button