ATCL kurejesha safari za Dar–Moscow Septemba 7

DAR ES SALAAM: Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetangaza kurejesha safari zake kati ya Dar es Salaam na Moscow kuanzia Jumatatu, Septemba 7, 2026, baada ya kukamilika kwa tathmini ya kawaida ya hatari kuhusu mazingira ya uendeshaji wa njia hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya ATCL, tathmini hiyo imefanyika kwa kushauriana na mamlaka husika, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kampuni wa kufuatilia na kutathmini usalama wa safari katika mtandao wake wote.

ATCL imesema huduma za safari hurejeshwa pale tathmini inapoonyesha kuwa mazingira yanaruhusu kuendelea kwa safari.

“Safari zinazohusika ni TC422 na TC423, huku abiria waliokuwa wameahirisha safari zao kutokana na kusitishwa kwa huduma hiyo wakiruhusiwa kupanga upya safari bila gharama ya ziada,” imeeleza taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button