Ajali yauwa 12 Mbeya
WATU 12 wamefariki dunia katika ajali ya basi lenye namba za usajili T.282 CXT aina ya Yutong lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Tabora kupitia Wilaya ya Chunya baada ya kuacha njia na kugonga gema na kisha kupinduka.
Waliopoteza maisha kati yao wanaume watano akiwemo dereva wa basi hilo Hamduni Nassoro Salum, wanawake saba miongoni mwao watoto wadogo wawili.
Taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Wilbert Siwa imeeleza kuwa watu 33 wamejuruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea eneo la Luanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya.
SOMA: Dk Mpango atoa maagizo kudhibiti ajali Mbeya
“Uchunguzi wa awali uliofanywa umebaini kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva kushindwa kulimudu gari lake kwenye eneo lenye mteremko na kona kali, imeeleza taarifa ya ACP Siwa.
SOMA: Waziri Mbarawa ataka utafiti ajali Mbeya