Waziri Mbarawa ataka utafiti ajali Mbeya

Waziri Mbarawa ataka utafiti ajali Mbeya

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ameitaka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kuhakikisha wanafanya utafiti katika eneo la

Shamwengo karibu na kituo cha mafuta Inyala, mkoani Mbeya, ili kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara eneo hilo.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo jijini Dodoma, wakati wa kikao Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji kutoka kwa

Advertisement

Wakala huo na Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) zilizowasilishwa leo bungeni jijini humo.

“Ni kweli hapa changamoto zimekuwa kubwa katika eneo hilo na serikali haifumbii macho ajali zinazoendelea kutokea kwenye eneo hilo, sasa TANROADS fanyeni tafiti, ili kupata majibu ya haraka kutatua changamoto hii,” amesema Prof. Mbarawa.

Amesisitiza Wakala huo kuhakikisha wanaweka alama za barabara kwenye miundombinu hiyo, ili kupunguza gharama za matengenezo ya mara kwa mara pindi inapoharibika.