‘Wekeni utaratibu kusikiliza kero za wananchi’

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amekerwa na baadhi ya watendaji kushindwa kutatua kero za wananchi kwa wakati, hali inayowalazimu kuwatafuta viongozi wa ngazi za juu akiwemo Rais.

Kufuatia hali hiyo, Mrindoko amewataka viongozi wote mkoani humo kujiwekea utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi na baada ya hapo apate ripoti ya hali ya migogoro na utatuzi wake kila baada ya mwezi mmoja, ili kumsaidia Rais kutatua changamoto zilizo ndani ya uwezo wao kabla hazijamfikia.

Akizungumza katika kikao kazi na watendaji mbalimbali wa taasisi za serikali wakiwemo watendaji wa kata, vijiji, maofisa tarafa, wenyeviti wa mitaa na wenyeviti wa halmashauri, RC Mrindoko amesema viongozi hao kushindwa kuwa karibu na wananchi kumesababisha baadhi ya kero zilizotakiwa kutatuliwa ngazi hizo kufikishwa kwa viongozi wa TAMISEMI hadi Ikulu, jambo ambalo hakupendezwa nalo.

Amewataka viongozi hao kuwa waadilifu kwa kutenda haki pale mwananchi anapofikisha malalamiko, kujiepusha na vitendo vya rushwa ili wananchi wawe na imani na uongozi wao hasa kunapotolewa suluhu ya jambo fulani.

Pia amewataka viongozi hao kuwa karibu na wananchi, ili kurahisisha wananchi kufikisha kero zao kwa kwa wakati kabla hawajachukua uamuzi wa kuwatafuta viongozi wa ngazi za juu.

Habari Zifananazo

Back to top button