Mkakati wa Kudumu Utatuzi Migogoro ya Ardhi waandaliwa

DODOMA; Serikali imesema imeandaa Mkakati wa Kudumu Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Agosti 26, 2026 na Naibu EWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Asha Baraka aliyehoji lini serikali itaunda tume itakayotatua migogoro ya ardhi nchi nzima.

“Mkakati huu utawezesha kuwa na kanzi data moja ya Serikali inayohusu migogoro ya ardhi ili kuondoa ushughulikiaji wa mgogoro mmoja na taasisi zaidi ya moja na kuwa na uamuzi unaofanana.

“Hatua hiyo itaimarisha uelewa, uwazi, uwajibikaji na kasi katika kushughulikia migogoro ya ardhi, kuchochea, kuimarisha amani, umoja na mshikamano katika jamii na kuboresha mazingira ya uwekezaji katika ardhi na kukuza uchumi wa nchi,” amesema na kueleza kuwa mkakati huo utakapokamilika utatumiwa na taasisi zite husika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button