QATAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ametembelea kituo kikubwa cha kujitolea cha Qatar kinachojishughulisha na kutoa misaada kwa wenye mahitaji mbalimbali -Qatar Charity na kujionea shughuli zinazofanywa na kituo hicho.
Dk. Mwinyi ameonesha kufurahishwa na mapokezi mazuri aliyopata yeye na ujumbe wake na amevutiwa na kazi kubwa inayofanywa na kituo hicho chenye kusaidia wenye mahitaji hasa Yatima na wale walio katika nchi mbalimbali zikiwemo zenye mizozo sehemu mbalimbali duniani.
Miongoni mwa nchi zinazonufaika na misaada hiyo ni Tanzania ambapo wanaofisi yao jijini Dar-es-salaam na kuwataka kupanua zaidi shughuli zake za utoaji wa misaada katika maeneo mengine ya Tanzania