ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Doha,Qatar ambapo anatarajia kushiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa kutimiza miaka Thelathini ya Familia Duniani utakaofanyika 29 Oktoba 2024 nchini humo.
Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad, Rais Dk.Mwinyi na ujumbe wake wamepokelewa na viongozi waandamizi wa Qatar wakiongozwa Youssef Al Harami na Balozi wa Tanzania nchini Qatar,Balozi Habibu Awesi Mohamed.
Ushiriki wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi katika mkutano huo mkubwa wa Kimataifa utaongeza chachu ya Ustawi wa Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Comments are closed.