Ubomoaji Kikwajuni waanza kupisha mradi wa Infinity Hills

Zanzibar: Ubomoaji umeanza katika eneo la Kikwajuni lililotengwa kwa ajili ya mradi wa matumizi mchanganyiko wa Infinity Hills, ikiwa ni hatua muhimu baada ya kukamilika kwa malipo ya fidia kwa wakazi wa eneo hilo.

Mwekezaji, Infinity Developments, amethibitisha kuwa fidia yenye thamani ya mabilioni ya shilingi imeshalipwa kwa wakazi walioathirika, na hivyo kufungua njia kwa ujenzi wa mradi huu mkubwa kuanza.

Infinity Hills inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika maisha ya mijini Zanzibar, ikiwa na mpango wa kutoa zaidi ya nyumba 1,100 vya kisasa vya kuishi pamoja na mchanganyiko wa biashara na huduma za mtindo wa maisha.

Nyumba za makazi zinazobomolewa Kikwajuni

Ofisa mwandamizi wa kampuni hiyo alisema kukamilika kwa fidia ilikuwa hatua muhimu kuhakikisha mradi unaendelea kwa njia ya haki na shirikishi.

Soma: Mapinduzi sekta makazi mradi wa dola mil 250 ukizinduliwa Zanzibar

“Tunafurahi kuthibitisha kwamba majukumu yote ya fidia kwa wakazi wa awali yametimizwa. Hicho kilikuwa kipaumbele kwetu kuhakikisha mradi unaendelea kwa uwazi na uwajibikaji,” alisema afisa huyo.

Kuanza kwa kazi za ubomoaji kunaashiria kuingia katika awamu ya ujenzi, ambayo inatarajiwa kuzalisha mamia ya ajira kwa jamii za jirani, Wazanzibari na Tanzania kwa ujumla.

Afisa wa serikali anayefahamu mradi huo alimsifu mwekezaji kwa mtazamo wake, hususani katika kushughulikia fidia na ushirikishwaji wa wadau.

“Kiwango cha taaluma na ushirikiano kilichoonyeshwa na mwekezaji kimekuwa cha kupongezwa. Mchakato umeonyesha dhamira ya wazi ya kufanya kazi kwa karibu na mamlaka na kuhakikisha wakazi walioathirika wanatendewa haki,” alisema afisa huyo.


Baadhi ya wakazi a eneo hilo wameonyesha matumaini kuhusu maendeleo hayo.

Mkazi mmoja, aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema fidia imempa fursa ya kujenga upya maisha yake.

“Fidia imenisaidia kuhama na kutulia sehemu nyingine, na ninashukuru kwamba mchakato umekamilika. Unatupa mwanzo mpya,” alisema mkazi huyo.

Mkazi huyo aliongeza kuwa kuna matumaini kuwa mradi utaleta manufaa mapana kwa jamii inayozunguka eneo hilo.

“Tunatumaini maendeleo haya yataleta ajira na kuboresha miundombinu. Hicho ndicho kilicho muhimu zaidi kwa sasa,” alisema.

Ukikamilika, mradi huu unatarajiwa kuanzisha kiwango kipya cha maisha ya mijini Zanzibar, ukijibu mahitaji yanayoongezeka ya nyumba za kisasa na maendeleo jumuishi.

Ukiwa umebuniwa kuendana na dira ya muda mrefu ya Zanzibar ya maendeleo ya miji, Infinity Hills utachanganya makazi, biashara na huduma za mtindo wa maisha ndani ya eneo moja.

Ujenzi unatarajiwa kuchukua takriban miaka miwili, huku mwekezaji akionyesha kuwa ataendelea kufanya kazi kwa karibu na mamlaka na wadau kuhakikisha utekelezaji unaenda vizuri.

Mradi huu ni miongoni mwa uwekezaji kadhaa wa kiwango kikubwa unaounda mwelekeo mpya wa miji Zanzibar na kusaidia mabadiliko mapana ya kiuchumi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. ng.yandaz.com

  2. thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. gh.yandaz.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button