Rais Dkt Mwinyi awasili Jakarta

INDONESIA : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili jijini Jakarta na ujumbe wake akiwemo mkewe Mama Mariam Mwinyi.

Katika uwanja wa ndege wa Ngurah Rai, Bali Rais Dk.Mwinyi aliagwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje Indonesia, Balozi Acep Somantri pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Moshe Tembele.

Rais Dk. Mwinyi alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Indonesia na Afrika 2024, ambao umehitimishwa jana tarehe 03 Septemba 2024, katika hoteli ya Mulia, Bali Indonesia.

Akiwa jijini Jakarta,Rais Dk. Mwinyi atatembelea mashamba ya mwani, Kiwanda cha  Kuchakata Mafuta ya Karafuu pamoja na Bandari.

SOMA : Mauzo Tanzania na Indonesia yameongezeka

SOMA : Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amebainisha kuwa uhusiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Indonesia umekuwa maradufu ikizingatiwa ongezeko la thamani ya mauzo ya nje kutoka Tanzania kwenda Indonesia

Habari Zifananazo

Back to top button