Wadau watoa maoni urasimu sekta binafsi

DAR ES SALAAM: Mmoja wa wawekezaji katika sekta ya afya nchini Dk.Mahmood Mringo, ameishauri Serikali kufanya mageuzi makubwa ya kisera ili kunusuru sekta binafsi, akilalamikia utitiri wa kodi, mlolongo wa mamlaka za udhibiti, na riba kubwa za benki zinazokwamisha uwekezaji.

Mringo aliwasilisha malalamiko hayo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia (PPP Centre), David Kafulila, wakati wa Kongamano la Kitaifa la PPP katika Sekta ya Afya lililofanyika katika Chuo Kikuu cha MUHAS.

Akiwasilisha kilio hicho, Mringo alimtaka Kafulila kufanyia kazi changamoto zao ili kutekeleza programu ya PPP katika sekta ya afya.

Pia kutatua changamoto zao ametaka kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi, Mringo aliishauri Serikali kuanzisha utaratibu wa kutoa dhamana kwa wawekezaji wa afya ili wapate mikopo yenye riba nafuu.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button