Dk Nyansaho aipongeza SUMAJKT kwa kutoa ajira kwa vijana

DAR ES SALAAM: Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk Rhimo Nyansaho amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana hapa nchini.

Dk Nyansaho ameyasema hayo Julai 06, 2026 alipotembelea banda la JKT kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Dar es Salaam.

Amesema kuwa Kampuni tanzu za SUMAJKT zimekuwa zikitoa mchango mkubwa wa kupunguza ombwe la ajira kwa vijana hapa nchini, akitolea mfano Kampuni ya usafi na Unyunyizi dawa ambayo imetoa ajira kwa vijana wa kitanzania zaidi ya 4000.

Aidha, Dk Nyansaho amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake ya ulinzi na uzalishaji mali, katika kuhakikisha Taifa linakuwa salama na wananchi wanatekeleza majukumu yao kwa amani.

Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kutembelea banda la JKT ili kufahamu shughuli zote zinazotekelezwa na Jeshi hilo kupitia Vikosi, Makambi, Shule, Chuo na huduma na biashara zinazofanywa na kampuni Tanzu za SUMAJKT.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button