Rais Samia kuzindua mpango wa Mkumbi

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua taarifa ya Tathimini ya Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) jijini Dar es Salaam kesho.

Aidha Rais Samia ambaye atawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, atazindua taarifa ya hali ya uwekezaji nchini ya mwaka 2023, mwongozo wa uanzishaji na uendeshaji wa kanda maalum za kiuchumi nchini, pamoja na mpango mkakati ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Akizungumza jijini Arusha na waandishi wa habari , Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa ,Kitila Mkumbo amesema serikali ilianzisha mpango huo Juni 2019, kwa lengo la kufanya uchambuzi wa kina wa mazingira ya biashara nchini.

SOMA: Rais Samia kuzindua ripoti ya tafiti afya ya uzazi na mtoto

Amesema mpango huo ulilenga kuainisha mageuzi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kutatua changamoto na kuboresha mazingira ya kufanya biashara pamoja na uwekezaji nchini.

“Mkumbi imefanikiwa kuainisha maeneo makubwa matatu ya kushughulikia uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini, ikiwemo gharama za kufanya biashara,mlolongo mgumu na mrefu wa kupata vibali vya kufanya biashara na uwepo wa utitiri wa mamlaka za udhibiti zinazoratibu shughuli za biashara nchini,” amesema Profesa Mkumbo.

SOMA: Rais Samia kuzindua jengo la Papu Arusha

 

Habari Zifananazo

Back to top button