Rais Samia kuzindua ripoti ya tafiti afya ya uzazi na mtoto

Rais Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuzindua ripoti ya tafiti ya afya ya uzazi na matoto na viashiria vya malaria ya mwaka 2022.

Tafiti hiyo hufanyika nchini kila baada ya miaka mitano kupitia Ofisi za Mtakwimu Mkuu wa Tanzania Bara na Zanzibari kwa kushirikiana na Wizara za Afya pande zote mbili na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Aidha tafiti hiyo huongoza tathmini ya uwajibikaji katika kutatua changamoto za utoaji wa huduma za afya uzazi kwa kupima viashiria vilivyopo na jinsi tulivyofikia malengo ya utoaji wa huduma bora za afya ya uzazi pamoja na kupunguza au kuondokana na athari zitokanazo na changamoto za afya ya uzazi.

Sambamba na uzinduzi wa ripoti, Rais Samia anatarajiwa pia kuzindia magari ya kubebea wagonjwa, magari ya usimamizi pamoja na kugawa vifaa tiba nchi nzima ikiwa ni muendelezo wa azma yake ya kuboresha huduma za afya nchini.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button