Ujenzi Akademi ya Michezo Malya wafikia asilimia 55

DODOMA; Serikali imesema hadi kufikia Agosti, 2026 ujenzi wa Akademi ya Michezo Malya umefikia asilimia 55.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ametoa kauli hiyo bungeni leo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Ali Mzee aliyehoji serikali ina mkakati gani wa kuanzisha academy maalumu, ili kuibua vipaji kwa watoto kutoka shuleni.

“Serikali ina mpango wa kujenga shule maalumu 56 za michezo nchini, ambapo kila mkoa unatarajiwa kuwa na angalau shule mbili. Kwa sasa serikali ipo hatua ya kumtafuta mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa shule saba za michezo, ikiwa ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo.

“Serikali inaendelea na ujenzi wa Akademi ya Michezo Malya, ambayo jukumu lake la msingi litakuwa ni kulea na kuendeleza vipaji vya michezo vya watoto na vijana kwa misingi ya kitaalamu, ambapo hadi kufikia mwezi Agosti 2026 ujenzi wa akademi hiyo umefikia asilimia 55,” amesema Waziri Makonda.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

  2. Home cash earning job to earns more than $220 per Hour!** getting paid weekly more than 4700+Dollar per week or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. **Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA…
    .
    Here is I started_____ ⫸ http://Www.Cash54.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button