Waandishi Waonesha Ubunifu SKA 2026

WAANDISHI wa habari nchini wameonesha uwezo wa kuibua masuala mbalimbali ya maendeleo, kiuchumi na kimazingira kupitia kazi zao zilizowasilishwa katika Tuzo za Uandishi wa Habari na Makala za Maendeleo Samia Kalamu Awards (SKA) 2026.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upigaji kura jijini Dar-es-salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari (TAMWA) ambaye pia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Uandishi wa Habari na Makala za Maendeleo Samia Kalamu Awards (SKA) 2026 Dk. Rose Reuben amesema mwaka huu mwamko umekuwa mkubwa na kutarajia ushindi utakaopatikana kila mmoja ataweza kushinda kwa kazi zake.

Amesema kwa kufuata vigezo vilivyowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, kazi kubwa imefanyika katika kuchambua kazi hizo. “Amesema majaji walitazama kazi zilizowasilishwa kwa kufuata vigezo vilivyowekwa na kuweka alama kwa taarifa au kazi zilizofanya vizuri” alisema Dk Rose.
Ameongezea kuwa idadi ya kazi ya Makala zilizowasilishwa ilikuwa kubwa kuliko zilizofanikiwa kupita, kwa kuwa majaji walizingatia vigezo vilivyowekwa katika kuchagua kazi zilizofanya vizuri. Miongoni mwa makundi yaliyoongoza kwa idadi kubwa ya kazi zilizowasilishwa ni afya, ambapo zilifikia 279, ikifuatiwa na jinsia, wanawake na makundi maalumu yaliyokuwa na kazi 225 huku kundi la mazingira lilikuwa na kazi 180, elimu kazi 150, huku kundi la ardhi likiwa na kazi tatu zilizowasilishwa. SOMA: Ushiriki ‘Samia Kalamu Awards’ wasogezwa mbele



