Wakulima wa mahindi walenga magunia 20 kwa ekari

IRINGA: WAKULIMA wa kata ya Magulilwa wilayani Iringa wanatarajia kuongeza uzalishaji wa mahindi kutoka wastani wa gunia tano hadi zaidi ya 20 kwa ekari, baada ya kuanza kupata mbegu bora kwa bei ya ruzuku, hatua wanayoamini itabadilisha uzalishaji na kuongeza kipato cha kaya.

Kwa miaka kadhaa, wakulima katika eneo hilo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mbegu zenye ubora na gharama nafuu za pembejeo, hali iliyowafanya baadhi yao kutumia mbegu za kawaida ambazo, kwa mujibu wa viongozi wa eneo hilo, zilichangia mavuno kuwa madogo.

Sasa matumaini mapya yameibuka baada ya wakulima kuanza kutumia mbegu bora, huku wakitarajia kuvuka kwa kiasi kikubwa kiwango cha uzalishaji walichokuwa wakikipata hapo awali.

Afisa Kilimo wa Kijiji cha Mlanda, Neema Alex, amesema tofauti kubwa inayotarajiwa ni katika tija ya shamba, akieleza kuwa mkulima aliyekuwa akipata gunia tano kwa ekari anaweza kuongeza mavuno kwa kiwango kikubwa kwa kutumia mbegu bora pamoja na kuzingatia kanuni nyingine za kilimo.

“Kwa kutumia mbegu za kawaida tulikuwa tunapata mavuno madogo. Lakini kwa sasa tumepata mbegu bora zinazotolewa kwa ruzuku, tunatarajia uzalishaji uongezeke zaidi, kutoka gunia tano hadi gunia 20 na kuendelea kwa ekari,” amesema.

Amesema ongezeko hilo likitimia litakuwa na athari zaidi ya uzalishaji wa chakula, kwani litampa mkulima uwezo wa kupata ziada ya mazao ya kuuza na kuongeza kipato cha familia.

Mavuno yanapoongezeka, mkulima anapata nafasi ya kutenga sehemu kwa matumizi ya familia na kuuza sehemu nyingine, huku mapato yakisaidia kugharamia mahitaji kama elimu, afya, chakula na shughuli nyingine za kaya.

Diwani wa Kata ya Magulilwa, Boazi Mbilinyi, amesema eneo hilo lina wakulima wenye mashamba makubwa, baadhi yao wakimiliki hadi takribani ekari 50, lakini uzalishaji hauendani na ukubwa wa maeneo hayo.

“Wananchi wetu wamekuwa wakijishughulisha sana na kilimo, lakini changamoto kubwa ilikuwa gharama za pembejeo, ikiwemo mbegu na mbolea. Tunapoondoa baadhi ya vikwazo hivi, mkulima anaweza kuongeza uzalishaji na kipato,” amesema.

Mbilinyi amesema hapo awali baadhi ya wakulima walikuwa wakinunua mbegu kwa bei zilizokuwa kati ya Sh15,000 na Sh20,000, kulingana na aina na upatikanaji wake, hali iliyoongeza gharama za kuanzisha msimu.

Kwa sasa, amesema, mbegu za Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) zinazotolewa kupitia mpango wa ruzuku zinapatikana kwa bei nafuu zaidi, jambo linalowawezesha wakulima kupata mbegu bora bila kubeba mzigo mkubwa wa gharama.

Mbali na mahindi, wakulima wanaweza kupata mbegu za mazao mbalimbali, ikiwemo mpunga, alizeti na ufuta, kulingana na mahitaji ya maeneo husika.

Mkurugenzi wa Mgongolwa Agrovet and Seeds ambao pia ni wakala wa mbegu hizo za serikali, Joseph Mgongolwa amesema kwa wakulima wa Magulilwa na maeneo mengine, suala kubwa sasa si kupata mbegu pekee, bali kuhakikisha mbegu hizo zinatumika pamoja na mbinu bora za kilimo ili matarajio ya kuongeza mavuno yawe matokeo halisi mashambani.

Amesema kwa upande wao wanaendelea kuhakikisha mbegu zinawafikia wakulima kwa wakati na katika maeneo yao ili kuondoa changamoto ya wakulima kukosa mbegu bora wakati wa msimu wa kupanda.

Habari Zifananazo

13 Comments

  1. Migogoro ya mitihani ya kitaifa – Maandamano makubwa ya wanafunzi yalilenga madai ya udanganyifu/uvujaji wa mtihani wa NEET, pamoja na kasoro katika mitihani na utoaji wa matokeo ya CBSE. Waandamanaji walidai uwajibikaji na mageuzi katika mfumo wa mitihani

  2. Kutaka Waziri wa Elimu ajiuzulu – Waandamanaji walimtaka Waziri wa Elimu wa Muungano, Dharmendra Pradhan, awajibike kutokana na migogoro hiyo. Hatimaye alijiuzulu tarehe 25 Julai 2026.

  3. Ajira na mustakabali wa vijana – Vijana wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa ajira na fursa, jambo lililosaidia kuifanya harakati hiyo kuwa pana zaidi ya suala la mitihani.

  4. Mwinuka: Ni kwamba malalamiko uliyowasilisha hapa Mahakamani yanahusu wagombea wa Serikali za Mitaa 2019? says:

    Sera za wafanyakazi – Pia kumekuwa na maandamano makubwa ya wafanyakazi kupinga sera zinazodaiwa kudhoofisha haki na maslahi ya wafanyakazi; tarehe 12 Februari 2026, mamilioni ya wafanyakazi walishiriki mgomo wa kitaifa.

  5. Masuala ya kisiasa na sheria – India imekuwa na historia ya maandamano makubwa kuhusu sheria za uraia, sera za Serikali, rushwa, haki za kijamii na masuala ya kidini. Kwa mfano, maandamano ya Citizenship Amendment Act (CAA) ya 2019 yalivuta mamia ya maelfu ya watu.

  6. Mwinuka: Mtu akiwa na malalamiko dhidi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, atakuwa sahihi kupeleka wapi? Mahakama ya Wilaya au wapi? says:

    Vita vya Iraq (2003): Kupinga uvamizi wa Iraq ulioongozwa na Marekani na washirika wake. Waandamanaji wengi walipinga vita na madai kwamba Iraq ilikuwa na silaha za maangamizi.

  7. Salt March / Dandi March (1930): alipinga ukoloni wa Uingereza na kodi ya chumvi, akitumia maandamano yasiyo ya vurugu.

  8. Hong Kong (2019): Kuanza kulipinga muswada wa uhamishaji wa washukiwa kwenda China, kisha madai yakapanuka hadi uhuru wa kisiasa na demokrasia zaidi.

  9. Arab Spring (2010–2012): Hasira kuhusu utawala wa kimabavu, ukosefu wa ajira, ufisadi, kupanda kwa gharama za maisha na ukosefu wa uhuru wa kisiasa.

  10. India (2019–2020): Kupinga Sheria ya Uraia (CAA) na hofu kwamba sheria hiyo ingeweka ubaguzi wa kidini katika upatikanaji wa uraia.

  11. Black Lives Matter (2020): Kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi, hasa baada ya kifo cha George Floyd akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

  12. Maandamano ya COVID-19: Sababu zilitofautiana; baadhi zilipinga lockdown, vizuizi vya safari, ulazima wa chanjo au sera nyingine za afya ya umma.

  13. Venezuela (2017): Kupinga serikali ya Nicolás Maduro, hali ya uchumi, ukosefu wa bidhaa na huduma, pamoja na migogoro kuhusu demokrasia na mamlaka ya taasisi za serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button