Marekebisho ya sheria kugusa sura ya jinai kwa watumishi

DODOMA; Serikali imewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026) ambapo sheria 21 zinapendekezwa kufanyiwa marekebisho.

Akiwasilisha muswada huo leo Septemba Mosi, 2026, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari ametaja miongoni mwa sheria zinazopendekezwa kurekebishwa ni Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20.

“Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 4 kinapendekeza kurekebishwa kwa kuondoa masharti yanayoweka ulazima wa shauri lenye sura ya jinai, madai au utawala chini ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 na Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 kushughulikiwa kwanza katika utaratibu wa madai au wa kiutawala kabla ya kuanza taratibu za jinai.

“Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kuhakikisha kuwa makosa ya jinai yanayotokana na masuala ya ajira yanashughulikiwa kwa wakati, hivyo kuwezesha upatikanaji wa haki jinai kwa wakati na kuondoa ucheleweshaji na ukosefu wa haki jinai kwa waathirika wa uhalifu,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button