Faida Azimio Mkataba uanzishwaji GGGI zatajwa

DODOMA; Serikali imewasilisha bungeni maelezo kuhusu Azimio la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Taasisi ya Ukuzaji wa Maendeleo ya Kijani Duniani (GGGI).

Akiwasilisha bungeni maelezo ya kuhusu Azimio hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Yussuf Masauni, ameeleza faida mbalimbali endapo Tanzania Mkataba huo hilo.

“Chimbuko la Azimio la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Taasisi ya Ukuzaji wa Maendeleo ya Kijani Duniani ni Ibara ya 21 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Taasisi ya Ukuzaji wa Maendeleo ya Kijani Duniani inayotoa nafasi kwa nchi kujiunga na Taasisi ya Ukuzaji wa Maendeleo ya Kijani Duniani (Global Green Growth Institute (Taasisi ya GGGI)).

” Taasisi ya GGGI ni taasisi ya kimataifa inayowezesha nchi wanachama kutekeleza mipango ya maendeleo inayozingatia ukuaji wa uchumi wa kijani ili kufikia malengo endelevu na Makubaliano ya Paris kuhusu upunguzaji wa gesijoto,” amesema Waziri Masauni.

Ametaja baadhi ya faida Tanzania kuridhia mkataba huo ni kuongezeka kuimarika kwa uwezo wa kuibua na kuandaa miradi ya uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi;

“Kuongezeka kwa taasisi za ndani zenye ithibati katika usimamizi wa fedha za mifuko ya kimataifa ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa uwekezaji kwenye hati fungani za kijani;

“Kuongezeka kwa upatikanaji wa fedha za misaada na mikopo yenye riba nafuu kwa nchi;

“Kuongezeka kwa wigo wa kidiplomasia na ushawishi wa nchi katika medani za kisiasa, kiuchumi na uhifadhi wa mazingira, kuongezeka kwa upatikanaji wa fursa za ajira kwa watanzania;

“ Kuimarika kwa mbinu za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi kupitia tafiti; na kuongezeka kwa tija na uzoefu wa wataalamu wa ndani katika masuala ya ukuaji wa uchumi wa kijani,” amesema Waziri Masauni. BUnge limeridhia Azimio hilo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button