Gharama upimaji kiwanja kimoja Sh 130,000

DODOMA; Serikali imesema gharama za upimaji ardhi kwa maeneo ambayo yameendelezwa hutozwa kwa kuzingatia Mwongozo wa Urasimishaji wa mwaka 2021.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini, Dickson Lutevele aliyehoji lini serikali itaanzisha utaratibu wa kupima ardhi kwa bei nafuu kwa wanaanchi wa Kata za Isalavanu, Bumilaying, Rungemba na Saohili.

“Kwa mujibu wa mwongozo huo gharama za kupanga na kupima kiwanja kimoja ni shilingi 130,000.

“Kabla ya hatua za Serikali kupunguza gharama hizo, wananchi walikuwa wanalipa kati ya shilingi 250,000 hadi shilingi 400,000 kwa ajili ya upangaji na upimaji wa kiwanja kimoja.

“Kwa upande wa upimaji wa kawaida usiohusisha urasimishaji gharama za upimaji zinatozwa kupitia Mwongozo wa Ukadiriaji Bei za Viwanja wa Mwaka 2016, ambao umeweka vigezo vya gharama za upimaji kwa kutegemea umbali eneo lilipo, ukubwa wa eneo linalopimwa, umbali kutoka alama za msingi zilipo, idadi ya vifaa vya kufanyia kazi na gharama za alama za mipaka (Beacons) zinazohitajika,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button